Fahamu Miwani Zilizotengenezwa Maalum Kwa Watu Wafupi

Mbunifu, Bw. Dominic Wilcox ametegeneza miwani inayowawezesha watu ambao si warefu kuweza kuona kinachoendelea mbele kutokana na upeo wa macho yao kutoruhusu kwa sababu mbalimbali. 
Miwani hiyo inaitwa “One foot taller” ambayo inamuwezesha mtumiaji kuweza kuona kitu kilicho umbali wa karibu sentimita 30.5 zaidi kuliko uwezo wa macho yetu, inayowasaidia watu warefu kutokuwa kikwazo kwa wengine kutokana na walivyoumbwa (kuwa warefu) hivyo basi kufanya wale ambao wamewazidi urefu kushindwa kuoma kilicho mbele yao kwa mbali.

“Wazo la kutengeneza miwani ya ina hiyo lilikuja baada kwenda kwenye ukumbi wa starehe ambapo bendi moja ya muziki ilikuwa inatumbwiza kisha nikamuona mwanamke mmoja akicheza muziki lakini anashindwa kuwaona wahusika (wanaotumbwiza)”~Dominic Wilcox.
Lenzi za kwenye miwani hiyo zimetengenezwa kwa teknolojia moja ambapo ili ndogo imefunwa kwenye pembe ya nyuzi 45 na kile kikubwa kimewekwa kwa kupitisha kidogo usawa wa macho ya mvaaaji hivyo kuweza kutekeleza kile ambacho kimekusudiwa.EmoticonEmoticon