Kunuka
kikwapa ni tatizo kubwa katika mwili wa binadamu. Tatizo hili
husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu chini ya kwapa.
Sasa basi, kuna njia nyingi ambazo watu wengi huzitumia ili kwapa liwe na harufu nzuri, kavu na safi.
Sasa basi, kuna njia nyingi ambazo watu wengi huzitumia ili kwapa liwe na harufu nzuri, kavu na safi.
Wengine hutumia njia za
kisasa ambazo ni pamoja na kupaka doodoranti au pafyumu zinazosaidia kuondoa
harufu mbaya mwilini.
Lakini kama hiyo
haitoshi, kuna njia za kisasa zinazoweza kuzuia harufu ya kwapa ambazo ni
pamoja na kupaka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa
safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya.
Kuvaa nguo safi zenye
nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufi zitasaidia kufyonza unyevu na
kuliacha kwapa lako kuwa kavu, safi na bila harufu mbaya.
Kuoga kila siku na kusafisha
nguo kwa maji safi kunasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya.
Pia kunywa maji mengi
kila siku kunakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya
kwapa.
Njia nyingine
inayoshauriwa ni kuhakikisha kuwa unaosha kwapa mara kwa mara kwa kutumia
sabuni zenye dawa (medicated soaps).
Aidha, kupunguza kula
chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu. Inasemekana kuwa kula vitunguu vingi
kunachangia mwili kutoa harufu kali.
Licha ya pafyumu na spray
kusaidia kuondoa harufu mbaya mwilini, hii si dawa endelevu kwani baada ya muda
harufu inaweza kurudi palepale hivyo ni vema kutumia njia za asili kukabiliana
na hali hiyo. Pafyumu haiwezi kutibu tatizo moja kwa moja.
Pia inashauriwa kuwa
baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao
huwavutia bakteria kukua katika maeneo yaliyojificha (yenye mikunjo).
Mbinu nyingine ni
kujitahidi kunyoa nywele za kwapa mara kwa mara na kuepuka kukaa sehemu zenye
joto kupita kiasi kwa muda mrefu.
EmoticonEmoticon