Kinachozungumziwa ni namna ya
kujipandisha thamani ili mpenzi wako asikuchoke wala kukushusha au kukuona wa
kawaida. Kila wakati akuone wa muhimu na akufanye namba moja katika maisha
yake. Kabla sijafika hapo nataka kwanza mfahamu dalili atakazozionyesha
mwenzako zinazoashiria kuwa amekushusha thamani yako kwake.
(i) Mawasiliano hupungua
Hapa
inategemea na kasi ya mawasiliano mliyokuwa nayo mwanzo lakini kwa kiwango
chochote kile huanza kupungua. Kama alikuwa na kawaida ya kuwasiliana nawe mara
kwa mara akikueleza mambo mbalimbali – hata madogo tu, kuhusu mwenendo wa siku
yake, ataacha.
(ii) Msiri kupitiliza
Kulingana na
kiwango cha uhusiano wenu, ataanza kuwa msiri kwa baadhi ya mambo yake. Hata
kama anafanya jambo fulani zuri kwa ajili ya maisha yenu ya baadaye,
hatakuambia. Unaweza kushtukia tu kusikia kwa watu kuwa mwenzako ameagiza gari
au amenunua kiwanja mahali na pengine ameshaanza ujenzi bila kukujulisha.
(iii) Hukupuuza
Kama awali
alikuwa na kawaida ya kukusikiliza, sasa ataanza kukupuuza. Unaweza kumwambia
jambo lenye manufaa makubwa kwenu lakini asilichukulie umakini. Hii ni dalili
kwamba wewe huna thamani kwake.
Jambo La Ziada
Kama
umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa
ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa lakini kwa sababu
ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.
Ukiwa kwenye
ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na
hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanza. Haoni cha muhimu
tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi.
Itafikia
hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama
ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba
hamuendani humwingia.
Jambo La Kufanya
Kubwa
unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani
lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka
na kufikia hatua ya kukushusha thamani.
Tayari
tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo
makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo
inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.
EmoticonEmoticon