Fifa Yaipa Manchester City Adhabu Ya Kulipa Faini, Man City Wakubaliana Na Adhabu Hiyo

Klabu ya Manchester City imepigwa faini ya pauni elfu mia tatu baada ya kupatikana na hatia ya kuwanunua wachezaji wenye umri mdogo pamoja na usajili wa wachezaji kutoka mataifa mengine. 

Klabu ya Man-City ilipatikana na hatia ya kuvunja sheria ya kumi na tisa ya Fifa kuhusu Usajili.

Kulingana na habari  iliyotolewa na shirikisho la soka duniani,FIFA klabu ya Manchester City ilikubali makosa yote iliyosemekana ilikuwa imefanya,” 


Klabu ya Manchester City inakubaliana na matokeo ya uchunguzi wa shirikisho la soka duniani FIFA na hivyo klabu hii ipo tayari kukubaliana na adhabu yoyote itakayotolewa na FIFA.”

Kesi ya Manchester City ni tofauti kidogo na kesi za awali kwani kwenye uamuzi wa kamati ya shirikisho City ilikubaliana na matakwa ya FIFA pamoja na kurahisisha mambo. Shirikisho hili limeamua kuwapiga Manchester City faini pekee.”

Awali klabu ya Chelsea ilipigwa marufuku katika kushirki kwenye dirisha la uhamisho kwenye madirisha mawili ya Usajili pamoja na faini ya pauni elfu mia nne. 

Kulingana na FIFA, Chelsea ilikataa matakwa ya FIFA yote jambo lililopelekea adhabu hio kali.
Hata hivyo, Klabu hio bado imo kwenye uchunguzi na shirikisho la UEFA kufuatia uvunjaji wa sheria kuhusu utumizi wa Fedha,(Financial fair Play).


EmoticonEmoticon