Uzuri wa
mapenzi ni kuridhishana. Kila mmoja ‘ainjoi’ kukutana na mwenzake, alifuarahie
tendo katika hali ambayo hawezi kuwa na hamu ya mapenzi pale anapokuwa
amemaliza tendo. Kinyume na hapo, kukiwa na tatizo katika
upande mmoja, furaha ya tendo inaondoka.
Mmoja kati ya wapendanao anakuwa
na shauku ya tendo wakati mwingine hana. Kitakachofuata hapo ni yule ambaye
hajaridhika kutafuta njia mbadala ili kupata tiba ya mapenzi. Kwa kizazi cha sasa,
watu wengi sana wamekuwa wakiteswa na tatizo la kutoridhishwa au kutomridhisha
mpenzi wake.
Mwanaume
anaweza kuwa anataka kumridhisha mpenzi wake, lakini anashindwa au mwanamke
anataka kumridhisha mpenzi wake, lakini inashindikana. Wanapokutana faragha,
kila mmoja anakuwa na nia njema kabisa kutaka kukamilisha tendo la ndoa, lakini
kwa tatizo linakuwa kwa mmoja wao na kuwafanya washindwe kufurahia tendo.
Mmoja kati ya wampendao anakuwa
anawahi kuridhika wakati mwenzake anakuwa bado hajafikia muda wa kuridhika.
Hapa ndipo zinapoibuka zile kauli za ‘mwenzangu haniridhishi’, ‘mwenzangu
amekuwa gogo’ na nyingine nyingi zinazofanana na hizo.
Yule ambaye
haridhishwi huwa anakuwa katika wakati mgumu. Kutokana na desturi ya watu
kutopenda kuambiana ukweli hususan katika jambo hili ambalo wengi wanaamini ni
la aibu, hubaki nalo moyoni na kuendelea kuumia. Anavumilia hadi inafika wakati
anachoka. Kinachofauta hapo ni kusaka suluhu. Ndiyo wakati wa kuanza kuwatafuta
marafiki tofautitofauti ambao wanaweza kumshauri vizuri au vibaya.
Wapo
wanaoweza kumshauri kwamba afanye vitu fulanifulani ili aweze kufanikiwa,
lakini wengine huweza kumshauri atafute mtu mwingine ambaye atamridhisha.
Kutokana na kero anayoipata, ni rahisi tu kufanya uamuzi wa kujaribisha kwa mtu
mwingine. Usaliti ndiyo unaanzia hapo. Amani inatoweka na baadaye ugomvi
huibuka, hapo ndipo watu hufikia hatua ya kushindwa kuvumiliana na hatimaye
kuachana.
NINI CHA KUFANYA?
Kinachotakiwa
kufanyika suala kama hili linapotokea, kwanza ni kuzungumza na mwenzako. Kama
unaona kuna kitu hakipo sawa kwa upande wako, mueleze mwenzako ili muweze
kutafuta suluhu. Kama pia tatizo unaliona lipo kwa mwenzako, tumia lugha nzuri
kumueleza ili muweze kupata suluhisho.
Yawezekana tatizo ambalo upo au
yuko nalo ni la kisanaa ya tendo. Tendo hili linapaswa kufanyika kwa sanaa na
ubunifu ili muweze kwenda sawa.
Yawezekana
mwenzako anakurupuka, kabla hajakuandaa yeye anakuwa tayari ameshafika mbali
kifikra hivyo kujikuta anakuacha kwenye mataa. Jadilini kwa kuelezana nini
kifanyike ili kila mmoja afurahie tendo. Elimu ya kujiandaa inabidi kila mmoja
aifahamu. Ushirikiano wa kulifanya tendo liwe na mashamsham linatakiwa.
Ujue wapi
mwenzako anapenda umguse zaidi na kwa namna gani. Ni vyema mkawekana wazi ili
kila mmoja asiwe mgeni na mwenzake. Ukimya wakati mwingine ndiyo unasababisha
matatizo ya wapendanao kutofautiana. Yawezekana ulilonalo au alilonalo mwenzako
ni la kitabibu, waweza kumshauri akaenda kutibiwa hospitalini na likaisha.
Mueleze mwenzako, mtashauriana na
kupata suluhu. Hakuna sababu ya kuhangaika kwa kutafuta suluhu ya kuridhishwa
na mtu mwingine. Unaweza kufanya hivyo kumbe nako bado ukakutana na tatizo ni
lingine. Utahamia kwa mwingine bila kujua kiini cha tatizo huenda ni wewe
mwenyewe, matokeo yake yatakuwa ni yaleyale.
Mheshimu
mwenzako. Mtunzie siri kwani faragha inahitaji siri. Mnapokuwa wawili,
elezaneni ukweli. Mueleze akutekelezee nini ili wewe uridhike. Kama kweli
mmepandana kwa dhati na mna ndoto ya kufika mbali, hakika mtashughulikia tatizo
na kusonga mbele.
EmoticonEmoticon