Jose Mourinho Amtaja Maguire Ndiye Mchezaji Bora Baada Ya Game Kati Yao Na Chelsea

Harry Maguire amethibitisha ubora wake baada ya  kucheza vyema mechi yake ya kwanza dhidi ya Chelsea Aug 11 usiku.
Jose Mourinho amemtaja Maguire ndiye mchezaji bora wa mechi hiyo ambayo Manchester United ilishinda mabao 4-0.
Maguire ametua Old Trafford katika usajili wa majira ya kiangazi akiwa ndiye beki ghali duniani akinunuliwa kwa Pauni80 milioni akitokea Leicester City.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England amempiku Virgil van Dijk wa Liverpool aliyekuwa beki ghali alipotua ndani ya klabu hiyo misimi miwili iliyopita akitokea Southampton kwa Pauni75 milioni.
Maguire aliituliza ngome ya Man United licha ya kucheza mechi yake ya kwanza tena yenye ushindani mkali.
Kocha huyo wa zamani wa Man United na Chelsea, alisema beki huyo wa kati alicheza kwa kiwango bora.


EmoticonEmoticon