Kauli Ya Ibrahimovic Kuhusiana Na Pogba Kutaka Kuondoka Man U

Mchezaji wa zamani wa Manchester Utd, Zlatan Ibrahimovic amesema klabu hiyo inatakiwa imuuze kiungo wake nyota, Mfaransa Paul Pogba.

Pogba anahusishwa kujiunga na Real Madrid pamoja na Juventus kwa uhamisho wa mapendekezo.
Zlatan alicheza na Pogba kwa mwaka na nusu alipokuwa Manchester Utd, huku akisema hakuna mchezaji ambaye anaweza akawa tofauti na malengo yake.
"Kama hataki kubaki haina haja ya yeye kubakishwa, kama anataka kwenda sehemu nyingine aachwe aende," alisema.
Alisema muda huu ni sahihi kupeleka mchezaji ambaye hatak kubaki na timu, mchezaji anatakiwa awaheshimu wenzake na kuelewa mazingira ya muda sahihi.

"Timu na uongozi zinakuwa na wasiwasi kwasababu ya mchezaji hataki kubaki, eti kisa hauwezi kupata asilimia fulani katika pesa," alisema Zlatan anayeicheza LA Galaxy ya Marekani inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini (MLS).


EmoticonEmoticon