Kikao Cha Maofisa Wa Barcelona Na PSG Kuhusiana Na Neymar Kurudi Barcelona

Maofisa wa PSG na Barcelona wamekutana kwa mara ya kwanza wakitumia saa tatu kujadili uhamisho wa staa wa kimataifa wa Brazil, Neymar, 27 ambaye anataka kurudi Nou Camp kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Septemba 2.
Hata hivyo, hakukuwa na makubaliano yaliyofikiwa ambapo inaaminika Barcelona ilitoa ofa ya Pauni 93 milioni na viungo wake wawili, Philippe Coutinho, 27, na Ivan Rakitic, 31, kwa ajili ya staa huyo lakini PSG wamegoma.
Inadaiwa ndani ya dili hilo PSG ilikuwa inataka aongezwe beki wa kulia wa kimataifa wa Ureno, Nelson Semedo, 25, lakini Barcelona imekataa mpango huo na inadaiwa mazungumzo hayo yataendelea tena siku chache zijazo.
Pia, inadaiwa PSG inataka pesa zaidi katika dili hilo ili iweze kumnasa mbadala wa Neymar ambaye macho yao yapo kwa Paul Dybala wa Juventus ambaye pia anawindwa na Tottenham kwa udi na uvumba.


EmoticonEmoticon