Kocha Wa Barcelona Asema Milango Ipo Wazi Kwa Mchezaji Mmoja Tu, Arudi Muda Wowote

Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde  ameacha mlango wazi kwa mshambuliaji Neymar kurejea katika kikosi hicho muda wowote anaotaka.

Valverde kila anapoulizwa kurejea kwa mchezaji huyo, amekuwa akitoa kauli ya kutopinga chochote ambacho kinakuja mbele yake siku za usoni kuhusu mchezaji huyo.

“Tutaona nini kitatokea lakini kwa hivi sasa yeye ni mchezaji wa timu nyingine, mimi ni kocha kitu ambacho nafikilia hivi sasa ni wachezaji niliokuwa nao,” alisema.
Aliongeza anatambua kazi ya ukocha ni kufundisha wachezaji hivyo hata suala la Neymar linaweza likatokea mbele, lakini hivi sasa hajui nini ambacho kitatokea.

Neymar anayekipiga katika klabu ya PSG nchini Ufaransa, anahusishwa mara kwa mara kurejea katika klabu yake ya zamani Barcelona.


EmoticonEmoticon