Kubwa La Kujua Kuhusiana Na Ulinzi Wa Whatsapp Kwenye Simu Yako

Siku za karibuni WhatsApp ilileta sehemu mpya ya ulinzi kwa alama za vidole kwenye program yake ya mfumo wa  iOs. 
Sasa hivi karibuni tegemea kupata sehemu hiyo kupitia simu za mfumo wa Android.

Sehemu hiyo itasaidia kuongeza ulinzi kwenye programu hiyo kwani kila mara ambapo utakuwa unataka kuingia kwenye programu hiyo, utaletewa ujumbe wenye kutaka kuweka alama ya kidole kupia sehemu hiyo ya fingerprint kwenye simu yako.


Pale mtumiaji anapowasha sehemu hiyo, mtu yoyote hatoweza kuona meseji zinazo ingia hata kama zikija kwa njia ya Notification au kupitia widget maalum inayowekwa juu ya kioo. 

Kama ikitokea mtu anataka kusoma meseji bila kuweka alama ya kidole basi ataletwa ujumbe ulio andikwa “content is hidden due to fingerprint lock”.
Vilevile kutakuwa na sehemu mpya ya mpangilio (Settings) ambayo itakuruhusu kuchagua ni wakati gani unapotaka sehemu hiyo iweze kujiwasha mara baada ya kumaliza kutumia programu hiyo. 

Unaweza kuchagua programu hiyo ijifunge yenyewe haraka unapo maliza kuchati na kufunga programu hiyo, au unaweza kuchagua ijifunge baada ya dakika moja au baada ya nusu saa.

Sehemu hii kwa sasa ipo kwenye programu ya majaribio ya WhatsApp Beta, na pengine tegemea kuona sehemu hiyo kwenye programu ya Android siku sio nyingi. 
Kama unayo programu ya majaribio ya WhatsApp unaweza kupata sehemu hiyo kupitia sehemu ya Settings kisha bofya sehemu ya Privacy alafu utaona sehemu ya Fingerprint Lock bofya hapo kuweza kuwasha sehemu hiyo.


EmoticonEmoticon