Kuna Madhara Gani Ya Kuhifadhi Vyakula Na Matunda Kwenye Friji?

Maisha ya mjini hasa barani Afrika kila mmoja yuko katika harakati za kujitafutia riziki na hali hii huwafanya watu wengi kujisahau kiafya.

Vyakula vinavyokaa kwenye jokofu kwa muda mrefu husababisha virutubishi huwa vinapungua.
Mtaalamu wa masuala ya Lishe Kasankala Ladislaus ,kutoka taasisi ya chakula na lishe nchini Tanzania (TFNC) anasema kuwa kuna athari ambazo zinaweza kupatikana kama mtu atahifadhi chakula chake kwenye jokofu kwa muda mrefu.
Uhifadhi wa vyakula kwenye jokofu unaweza kusababisha bakteria kuzaliana na kupelekea madhara kwa binadamu.
"Kuna bakteria ambao wanavumilia hali ya ubaridi na kuna bakteria ambao husababisha madhara kiafya".
Vyakula vibichi na vilivyopikwa vinafaa kuwekwa katika jokofu, lakini jambo la kuzingatia ni muda na upangiliaji wa chakula.
Kuna ngazi za upangaji wa vyakula

Vyakula vilivyoiva, vinapaswa kukaa juu zaidi na baada ya hapo ngazi inayofuata unapaswa kuweka samaki na baada ya hapo ni nyama na baada ya hapo kama unatumia nyama ya nguruwe ndio inafuata na ngazi ya chini kabisa ni mayai.

Upangaji huo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia bakteria mfano bakteria wa samaki wasiweze kujichanganya na bakteria wa kuku....au mfano bakteria wa nyama ya nguruwe ni hatari kuweza kuenea katika vyakula vingine kama haitahifadhiwa vizuri.
Lengo la uhifadhi wa vyakula kwenye jokofu ni kuwezesha vyakula hivyo visiharibike kwa muda.
Lakini huo muda wa kuhifadhi vyakula unapaswa kuzingatiwa.
Nyama, mchicha na samaki hazifai kukaa kwa muda mrefu...siku mbili au tatu inatosha.

Mkate unaweza kukaa hata siku saba mpaka utakapoanza kuonyesha vidoti vyeusi.
Vitunguu havishauriwi kuwekwa kwenye friji lakini kuna aina ya vitunguu vyekundu vinaweza kukaa hata mwezi mzima.
Mboga za majani na matunda zisikae kwa muda mrefu pia ni siku mbili au tatu.

Ni vyema kujua nyuzi joto ambayo unaweka katika jokofu lako (0-8).
Ni muhimu kuosha vizuri vitu unavyoweka kwenye jokofu na hata maji yanapaswa kuwa yamechemshwa kwa sababu jokofu inahifadhi lakini haiuwi vijidudu.


EmoticonEmoticon