Kuna Nini Tottenham Kwenye Kumsajili Philippe Coutinho?


Tottenham wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho kwa mkopo wa msimu mmoja.
Raia huyo wa Brazil amehusishwa na vilabu kadha vya ligi ya Premier. Coutinho alifurahia mkopo wa miezi 6 chini ya Mauricio Pochettino alipokua meneja wa Espanyol mwaka wa 2012, akifunga mabao 5 katika mechi 16.
Inaaminika kuwa ni timu chache tu ndio zina uwezo wa kufikia gharama ambayo Barca’s imemwekea Coutinho baada ya kulipa pauni milioni 142 January mwaka 2018. Kuwasili kwa Coutinho Tottenham kutaongezea fununu kwamba Manchester United wanatathmini kumsajili Cristian Ericksen.


EmoticonEmoticon