Maamuzi Ya Mahakama Baada Ya Kumkuta Asap Rocky Na Hatia

Mahakama nchini Sweden imemkuta na hatia rapper Asap Rocky na wenzake wawili kwenye kesi iliyokua ikimuandama  ya kumpiga na kumjeruhi shabiki mmoja nchini humo ambapo ishu hiyo ilitokea 30 June,2019.

Mahakama imeamua kutompa kifungo cha jela na kuamuru kuwa itabidi amlipe  fidia ya kiasi cha shilingi Milioni 3 za Kitanzania kijana huyo kutokana na kumjeruhi.

Mahakama imeamua kufanya hivyo kutokana na kudai kuwa Asap alisota rumande kwa muda na ugomvi huo haukusababisha maafa makubwa ya kufikia hatua ya kumpa kifungo.


EmoticonEmoticon