Mabeki 5 Waliogharimu Kiwango Kikubwa Cha Pesa Duniani Wakati Wote

Mchezo wa soka umejipata katika hali tatanishi ya kifedha na haswa inapofika wakati wa usajili kwani vilabu vingi vimekuwa vikiazimia kupata faida ya juu iwezekanavyo. Baada ya usajili wake Harry Maguire, kunao walinzi wengine waliosajili kwa bei ya kuishangaza Dunia.

1.Harry Maguire
Harry Maguire ndiye mlinzi ghali zaidi katika historia ya kandanda. Maguire alisajiliwa na Manchester United msimu huu akitokea Leicester City kwa kima cha millioni 85 huku akimpiku Van Dirk wa liverpool.
Maguire alichezea Leicester City mechi 69 huku akicheka na nyavu mara tano. Muingereza huyu mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuwa mmoja wa mabeki wa kutegemewa msimu ujao


2.Van Dijk
Liverpool ilishangaza wengi mwaka 2018 ilipomsajili mholanzi Virgil Van Dijk kutokea klabu ya southampton kwa kima cha millioni 75. Van Dijk alisaidia Liverpool kushinda taji la klabu bingwa msimu uliopita huku akiimarisha ngome ya Ulinzi ya wekundu hawa wa Anfield.
Kwa sasa Van Dijk ameichezea Liverpool mechi 72 huku akicheka na wavu mara saba. Van Dijk ana umri wa miaka 27.

3. Lucas Hernandez

Lucas Hernandez ni mlinzi wa kati ambaye pia ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kushoto anayetokea Taifa la Ufaransa. Hernandez alisajiliwa na FC Bayern Munich kutoka klabu ya Atletico Madrid kwa kitita cha millioni 68.
Hernandez alisaidia taifa lake la Ufaransa kutwaa taji la kombe la dunia mwaka uliopita nchini Urusi. Lucas kwa sasa ana umri wa miaka 24.

4.Matthijs De Ligt
Mholanzi mwingine kwenye orodha hii ni De Ligt aliyekamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Juventus akitokea Ajax amsterdam ya Uholanzi. Akiwa bado kijana mdogo mwenye umri wa miaka 20, De Ligt anatarajiwa kumrithi Leonardo Bonnuci mjini Turin.
Juventus ilimsajili De Ligt kwa kima cha millioni 67.5. Kabla kugura mjini Amsterdam, De Ligt alikuwa nahodha wao licha ya Umri wake mdogo.

5.Aymeric Laporte
Laporte ni mlinzi wa kati anayechezea klabu ya Manchester City. Pep guardiola alitumia kitita cha millioni 56 kumsajili Laporte kutoka klabu ya Athletic Bilbao ya Uhispania.

Msimu uliopita, Laporte alicheza mechi 35 msimu uliopita  kwenye ligi kuu nchini Uingereza Msimu uliopita. Aymeric kwa sasa ana umri wa miaka 25. Hata hivyo hajawahi chezea taifa lake mechi hata moja.


EmoticonEmoticon