Madhara Yatokanayo Na Bluetooth Ikisahaulika On

Bluetooth ni hatari sana kwa usalama na ni vyema kuacha kutumia teknolojia hiyo mara kwa mara hasa kwenye kwenye simu za mkononi.

Kwenye mkutano wa wadukuzi unaofanyika kila mwaka unaojulikana kama DEFCON, mkutano ambao unakutanisha wadukuzi mbalimbali kujadili maswala mbalimbali ya usalama wa mtandaoni. 

Kwa mwaka huu mkutano huo ulifanyika huko Las Vegas, Nevada kwa siku nne mfululizo.

Kupitia mkutano huo wadukuzi hao walionyesha jinsi wanavyoweza kutumia Bluetooth kuweza kudukua kifaa kama spika zenye kutumia teknolojia hiyo na kucheza nyimbo ambazo zinaweza kufanya mtu yoyote aliye karibu na spika hizo kupoteza uwezo wa kusikia.

Wadukuzi hao walionyesha jinsi wanavyoweza kuingilia mawasiliano yanayo fanyika kwa kutumia Bluetooth na kuweza kubadilisha data zozote zinazotumwa baina ya vifaa viwili vilivyo unganishwa kwa pamoja kwa kutumia Bluetooth.

Kupitia Airdrop, ambayo ni teknolojia ya bluetooth ya Apple wadukuzi hao wanaweza kupata data za muhimu kama vile namba kamili za simu za watumiaji wote wanaotumia sehemu hiyo.EmoticonEmoticon