Manchester United Washindwa Dau Analolitaka Paulo Dybala Wa Juventus

Man United imeamua kuachana na mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala katika uhamisho wa kubadilishana na Romelu Lukaku baada ya kushindwa kuhafikiana na mahitaji yake ya mshahara.

Dybala alitaka kulipwa kiasi cha Pauni 350,000 kwa wiki na United haipo tayari kumlipa staa huyo wa kimataifa wa Argentina dau hilo la mshahara na sasa itatazama mshambuliaji mwingine wa kuchukua nafasi hiyo.
Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer na mabosi wa United wanaamini staa huyo hana nia ya dhati ya kuichezea United na badala yake amejikita zaidi katika kutaka fedha kitu ambacho hawajavutiwa nacho.
Kutokana na hali hiyo United imeamua kukata kabisa mawasiliano na nyota huyo pamoja na wakala wake, ambao kwa upande wao wameamua kuufanya uhamisho wa nyota huyo kuwa dili.
Hata hivyo, klabu kibao za Hispania na Italia zingali zinahitaji huduma ya nyota huyo.


EmoticonEmoticon