Messi, Cristiano Ronaldo & Van Dijk Kuwania Tuzo Ya Mchezaji Bora

Mshambulizi wa Juventus na Ureno, Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji watatu waliochaguliwa kuwania tuzo la mchezaji  bora wa Ulimwengu msimu uliopita, Ballon D’Or.
Cristiano Ronaldo
Ronaldo alilisaidia taifa lake la Ureno kunyakua taji la UEFA Nations League huku akisaidia klabu yake ya Juventus kutwaa mataji matatu nchini Italia ikiwemo taji la ligi. Hata hivyo, Ronaldo alishindwa kuifikisha Juventus kwenye nusu nusu fainali za michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya.
Leo Messi
Lionel Messi alipeleka klabu yake ya Barcelona hadi nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya huku akicheka na wavu mara kumi na mbili. Messi pia alicheka na wavu mara 34 kwenye ligi kuu nchini uhispania alisaidia klabu yake ya Barcelona kutwaa taji la La liga na kombe la Copa Del Rey.
Hata hivyo Messi na taifa lake la Argentina kwenye awamu ya nusu fainali ya michuano ya Copa America.
Virgil Van Dijk
Mlinzi wa taifa la Uholanzi, Virgil Van Dijk amekamilisha orodha ya tatu bora baada ya kuisaidia klabu yake ya Liverpool kutwaa taji la klabu bingwa barani Ulaya.
Van Dijk pia alifikisha taifa lake kwenye fainali ya michuano ya UEFA Nations League ila walipoteza mchezo wa fainali mikononi mwa Ureno yake Cristiano Ronaldo.


EmoticonEmoticon