Movie Ya The Lion King Yafikia Mauzo Makubwa Kwa Muda Mchache Duniani Kote

The Lion King imekuwa filamu ya nne ya Disney mwaka huu kupata mauzo ya kiasi cha dola bilioni moja, yaliyopatikana baada ya kuuzwa kote duniani.
Filamu hiyo ya Disney ambayo awali ilitengenezwa mwaka 1994 imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha chini ya wikitatu baada ya kutolewa katika kumbi za sinema.
Sinema hiyo , ambayo ilijumuisha sauti ya Beyonce na Donald Glover, ambayo iliwahusisha wachezaji : Endgame, Captain Marvel na Aladdin n iliwekwa katika kitengo cha Desney cha filamu zilizopata mauzo ya dola bilioni 1 katika mwaka 2019.
Kulingana na Mkurugenzi sehemu ya Jon Favreau imekuwa ni ya tano kwa ukubwa katika orodha ya dunia ya filamu zilizokwishatolewa mwaka huu.
Katika Amerika Kaskazini mauzo yamepanda na kufikia karibu dola milioni 361 na mauzo ya dola milioni 638 yalipatikana katika nchi za kigeni, huku Brazili na Uchina zikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoitazama.
Muziki wakati wote ulikuwa ni sehemu kubwa ya ya mfanikio ya The Lion King , huku Sir Elton John akishindwa kuridhisha hadhira yake katika Tuzo ya Oscar kwa onyesho lake katika wimbo wake Can You Feel the Love Tonight.
Alilazimika kujitetea , mara mbili - katika nyimbo za The Circle of Life na Hakuna Mata -kupata tuzo ya wimbo bora wa kuimba mwenyewe.
Sasa nyimbo katika albamu ya Lion King zimekuwa katika 10 bora katika chati ya muziki bora wa Marekani , ukiwa nimradi ulioongozwa na kuandaliwa na Beyonce , The Gift.
Albamu yake aliyowashirikisha wasani mbali mbali - kama vile Kendrick Lamar, Pharrell Williams na wengine zaidi - ilipata alama 54,000 za albamu kwenye chati katika juma lililomalizika tarehe 25 Julai, kulingana na kampuni ya muziki ya Nielsen, na kwa sasa ni ya pili katika chati ya nyimbo bora zaidi 200 nchini Marekani.

Filamu mpya rasmi ya muziki ni ya pili kwa umaarufu kuwahi kurekodiwa katika aina hiyo ya muziki, ambapo iliuzwa mara mara 22,000 ,huku video ya muziki ya mwanzo ya Sir Elton, Tim Rice na Hans Zimmer ambaye alikamilisha onyesho aliloliita mzunguko wa maisha, ikiwa katika nafasi ya 150 , miaka 25 baada ya kutolewa kwa mara ya kwanza.


EmoticonEmoticon