Neymar Anataka Kuihama PSG, Klabu Yake Yathibitisha

Mshambuliaji wa PSG Neymar jnr hataichezea timu hiyo katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Nimes katika ligi ya daraja la kwanza nchini Ufaransa, huku mabingwa hao wa Ufaransa wakidai kwamba mchezaji huyo huenda akaihama klabu hiyo.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya PSG Leonardo amesema kuwa mazungumzo ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yamepiga hatua kubwa zaidi ya ilivyokuwa hapo awali.
Hatahivyo klabu hiyo haijatoa ruhusa yoyote ya uhamisho, alisema.
Mchezaji huyo ambye ndiye ghali zaidi duniani amehusishwa na uhamisho katika timu yake ya zamani ya Barcelona mbali na uhamisho mwengine wa Real Madrid.
Neymar alijiunga na PSG 2017 wakati klabu hiyo , iliokuwa ikimilikiwa na kampuni ya uwekezaji ya michezo nchini Qatar ilimlipa Neymar kitita cha £200m ili kumwezesha kujiondoa katika kifungu cha sheria cha kandarasi yake.
Mshambuliaji huyo amefunga magoli 34 katika misimu miwili akiwachezea mabingwa hao wa Ufaransa, ijapokuwa majeraha yameathiri vibaya kampeni yake.
Mkufunzi wa PSG Thomas Tuchel alisema kwamba Neymar alishiriki katika mazoezi siku ya Jumamosi lakini bapo alikuwa hajapona vizuri


EmoticonEmoticon