Pogba Afunguka Uhamisho Wake Kati Ya Juventus Na Real Madrid


Kiungo wa Manchester United Paul Pogba alisema kwamba bado kuna hali ya sintofahamu kuhusu hatma yake katika timu ya Manchester United licha ya ushindi wao mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili(Aug 11) katika mchuano wa kwanza wa ligi ya primia.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa ufaransa alitaka sana kuondoka Man United wakati wa likizo baada ya kukamilika kwa msimu wa ligi huku akihusishwa na uhamisho kujiunga na Real Madrid au Juventus.
Meneja Ole Gunner Solskjaer aliupongeza mchango wa Pogba baada ya kuandaa bao la tatu na la nne dhidi ya Chelsea, lakini kiungo huyo alisema “ni muda tu ndyo utakao amua” ikiwa atasalia nchini Uingereza.
“Mimi hujihisi vyema nikicheza soka. Nafanya vitu navyopenda, tena ni kazi. Najituma kila wakati nikienda uwanjani,” Pogba aliambia kituo cha radio cha Ufaransa RMC.
“Nafahamu kwamba kuna mambo ambayo yamesemwa. Ni muda tu ndyo utakaoamua. Bado patakuwepo alama ya duku duku.
“Niko katika timu ya Manchester. Nafurahia muda na wachezaji wenzangu. Kila wakati nataka kushinda mechi nami hufanya kadri ya uwezo wangu uwanjani.”
Kipindi cha uhamishi wa wachezaji kilifika tamati Alhamisi, siku moja kabla ya kuanza kwa msimu mpya, lakini vilabu nchini uingereza bado vinaruhusiwa kuuza wachezaji hadi kukamilika kwa kipindi cha uhamisho barani Eropa Septemba tarehe mbili.


EmoticonEmoticon