Polisi Waifunga Rasmi Kesi Iliyokuwa Inamwandama Rapa 50 Cent

Ile kesi ya 50 Cent dhidi ya askari Emanuel Gonzalez ambaye aliwahi kutoa amri kwa polisi kumpiga risasi rapper huyo punde tu akionekana popote? Sasa Kitengo cha mambo ya ndani mjini New York kimefunga rasmi uchunguzi wa shauri hilo.

Kwa mujibu wa New York Daily News, wapelelezi wamebaini kwamba amri hiyo ya Gonzalez ilikuwa masihara tu na hakumaanisha kama ambavyo 50 Cent aliipokea.

Baada ya kufungwa kwa kesi hiyo imemchukua masaa kadhaa tu kwa rapper huyo wa Marekani kuzungumza. Kwenye instagram yake amesema:
"Nilijua tu hawatofanya chochote juu ya hili hivyo ndio maana niliacha kulizungumzia. Idara ya polisi mjini New York inahusika kuyaficha makundi makubwa ya kihuni mjini humo. Inakupasa kuwa tayari kwa chochote." ameandika 50 Cent.


EmoticonEmoticon