Kuna baadhi ya wanawake
ambao hupata maumivu tofauti wakati wa siku za hedhi kila mwezi. Maumivu haya makali na mateso
huvuruga ratiba zao za kazi, kulea familia na hata kuacha kufanya shughuli za
kujiingizia kipato.
Wengi hutumia dawa na kupata nafuu, wengine hawapendi dawa
maana huleta madhara yasiyotegemewa mwilini na kulazimika kuvumilia mateso hadi
yanapoisha baada ya hedhi. Leo katika makala yetu tunaangalia jinsi ya
kupunguza maumivu ya hedhi kwa kuangalia vyakula vinavyoweza kutumika kama
dawa.
Vyakula ni
njia mbadala sababu hutumika kupunguza kiwango cha homoni au kemikali
zinazosababisha kuleta maumivu mwilini. Ili kuwa na uelewa mzuri, tuangalie
kiini cha tatizo hadi kusababisha maumivu makali wakati wa hedhi, halafu
tuangalie vyakula vinavyoweza kutatua tatizo.
CHANZO CHA TATIZO
Kemikali
aina ya prostaglandins ndio chanzo cha maumivu wakati wa hedhi kwa wanawake.
Kemikali hii hutengenezwa na chembechembe za mafuta yapatikanayo kwenye seli.
Kazi ya kemikali hii ni kusababisha uvimbe, kusinyaa kwa misuli, kusinyaa kwa
mishipa ya damu na kuganda kwa damu.
Muda mfupi
kabla ya kuanza hedhi, ukuta wa seli zinazotengeneza prostaglandins hujijenga
kwenye mji wa mimba. Wakati wa hedhi, seli hizi hubomoka na kusababisha
prostaglandis kutoka kwa wingi. Hii husababisha mishipa ya damu kusinyaa,
misuli kubana na kusababisha maumivu makali.
Kemikali za
prostaglandins huingia pia kwenye mfumo wa damu na kusababisha maumivu ya
kichwa, kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kuharisha.
Kiwango cha
prostaglandins ni kikubwa sana kwa wanawake wanaopata maumivu wakati wa hedhi
kuliko wale wasiopata maumivu.
Wanawake
wengi wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango hupunguza pia maumivu ya hedhi
sababu vidonge huzuia ukuaji wa seli zinazozalisha prostaglandins. Lakini
inawezekana pia kufikia malengo kwa kuangalia aina za vyakula.
VYAKULA VIPUNGUZAVYO MAUMIVU
Vyakula
vinaweza kufanya kazi ya kupunguza mauvimu ya hedhi kwa kurekebisha kiwango cha
homoni ya oestrogen mwilini.
Oestrogen ni
homoni ya kike inayotolewa mwilini kwa shughuli za kuzalisha seli. Oestrogen
hutolewa kwa viwango tofauti kutegemeana na muda wa mzunguko wa mwanamke huzalishwa kwa wingi sana baada ya hedhi na muda mfupi kabla ya hedhi kuanza.
Ili kuweza kupunguza maumivu, ni vizuri kuzingatia: Punguza vyakula vyenye
mafuta. Vyakula vya mafuta husababisha oestrogen izalishwe kwa wingi,
hivyo kuzalisha seli nyingi zaidi kwenye mji wa mimba.
Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi
(fiber). Nyuzinyuzi husaidia kusafisha mwili kwa kuondoa oestrogen kirahisi
toka mwilini, hivyo kupunguza kiwango chake kwenye damu na kuzuia kukua kwa
seli kwenye mji wa uzazi.
Kula nafaka, mboga za majani na matunda kwa wingi.
Jamii hii ya vyakula ina nyuzinyuzi (fiber) inayotumika katika kupunguza
kiwango cha oestrogen mwilini pia kunywa juisi za matunda halisi.
Acha kunywa
pombe au kula vyakula vya kusindika, visivyo asili maana huwa na mafuta mengi
yanayoweza kukusababisha matatizo zaidi. Kubadilisha vyakula inasaidia sana.
Wanawake wengi hufurahia matokeo na hata kuwaza kwa nini wasingefanya hili
zoezi mapema.
Kula chakula
bora na kupunguza uzito wa mwili ili uwe na afya bora. Ni muhimu kuzingatia
kula vyakula vya jamii ya nafaka, mboga za majani na matunda.
EmoticonEmoticon