Refa Wa Kike Kusimamia Mechi Kati Ya Chelsea Na Liverpool

Stephanie Frappart atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi ya UEFA super Cup baina ya Chelsea na Liverpool itakayochezwa tarehe kumi na nne mwezi Agosti mwaka huu ugani Besiktas Park Instanbul nchini Uturuki.
Stephanieni mwanamke mwenye umri wa miaka 25  na alikuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia kwa wanawake baina ya U.S.A na Uholanzi. 

Wasaidizi wake watakuwa Manuela Nicolosi kutoka Ufaransa pamoja na  Michelle O’Neal kutoka Jamhuri ya Ireland.
Mwezi Aprili, Stephanie aliweka historia kwa kuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke kupuliza kipenga kwenye mechi za ligi kuu nchini Ufaransa baada ya kusimamia mechi baina ya SC Amiens na RC Strausborg. 
Mwezi juni mwaka huu,Stephanie alitajwa kuwa mmoja wa waamuzi wa ligi kuu nchini Ufaransa mwezi ujao.


EmoticonEmoticon