Rick Ross Kuongezwa Kwenye Muendelezo Wa Filamu Ya Coming To America 2


Rick Ross ameongezeka kwenye orodha ya watu ambao wataungana na Eddie Murphy kwenye ujio mpya wa 'Coming To America' filamu ambayo iliiteka dunia miaka ya 80.

Rozay ametangaza kuwepo kwenye ujio huo mpya ambao pia Wesley Snipes ametangaza kushiriki. Nafasi ya ushiriki wa Rick Ross bado haijawekwa wazi huku utayarishaji wake ukitajwa kuanza hivi karibuni.
Kwenye mahojiano na Power 106 na Nick Cannon, Ross alisema sababu ya kukubali na kuamini kuwepo kwenye 'Coming To America' mpya ni kutokana na kurekodiwa kwenye mtaa wake mjini Atlanta na kuipenda sehemu ya kwanza iliyotoka June 26, 1988.


EmoticonEmoticon