Sajili Zilizokamilika Ndani Ya Dirisha La Uhamisho Aug 8

Dirisha la uhamisho la msimu wa joto la ligi ya EPL lilifungwa jana huku Romelu Lukaku akikamilish uhamisho wake kuelekea Inter Milan.
Rais huyo wa Ubelgiji aliwasili Italia kwa uchunguzi wa kimatibabu siku ya Jumatano na kukamilisha uhamisho wake San Siro hadi mwaka 2024. Lukaku alikua amehusishwa na uhamisho kuelekea Juventus awali.
Wakati huo huo Arsenal ambao walimsajili Kieran Tierney kutoka Celtic kwa pauni milioni 25, walikamilisha usajili wao na saini ya mlinzi wa Chelsea David Luiz.
Ni mchezaji wa sita kusajiliwa na Unai Emery msimu huu wa joto.
Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 26, amewasilisha ombi la kutaka uhamisho huku kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anapigiwa upatu kuhamia Everton.
Palace wameiambia Everton hawatakubali kupokea chini pauni milioni 100 kumwachilia mshambuliaji huyo. Hata hivyo uhamisho umekamilika na ingawa ataondoka msimu huu basi atakuwa akielekea nje ya Uingereza.
Bishara ya usajili ya dakika za lala salama ilipelekea fedha zilizotumiwa na ligi ya Premier msimu huu wa joto kufikia pauni bilioni 1.41, chini tu ya rekodi ya pauni bilioni 1.43 iliyowekwa mwaka 2017.
Fedha zilizotumika na vilabu vikuu vya Uingereza katika siku ya mwisho ya usajili zilifikia pauni milioni 170. Arsenal ndio waliotumia kitita kikubwa zaidi cha fedha Uingereza katika dirisha hilo kwa kutumia pauni milioni 155m kwa kumsajili David Luiz kutoka Chelsea kwa pauni milioni 8 dakika za mwisho.
Ligi ya EPL mwaka 2019/2020 inaanza usiku wa leo huku Liverpool ikichuana na wageni Norwich.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anaitaka timu yake kuwa na hasira na tamaa wanapojitayarisha kwa kipute hicho. Kiungo Sadio Mane atacheza licha ya kuanza matayarisho kuchelewa baada ya kuchezea Senegal katika kipute cha ubingwa bara Afrika.
Kiungo wa kati James Milner, aliyekosa Community Shield wikendi iliyopita baada ya kupona jeraha la msuli. Kesho mabingwa Manchester City watakabana na saa nane unusu mchana Arsenal wakipangiwa kuchuana na Newcastle jumapili.
Manchester United watapambana na Chelsea siku hiyo hiyo ugani Old Trafford.


EmoticonEmoticon