Ni maneno ya kawaida sana ambayo huenda
tunayasikia kila siku lakini nikuambie tu kwamba, kutamka maneno hayo kwa
mpenzi wako, nguvu yake ni kubwa sana.
Ikumbukwe uliye naye anataka mara kwa mara
kuhakikishiwa kwamba anapendwa, kwa maana hiyo kitendo cha wewe kila wakati
kumwambia NAKUPENDA kinamfanya ajisikie amani ndani ya moyo wake. Ndiyo maana
nakusihi sana usilipuuze neno hili pale inapobidi.
Lakini katika safari yenu ya maisha kuna
kukoseana. Unaweza kusema ama kufanya jambo likamkwaza mpenzi wako. Katika hali
hii kama kweli unampenda unachotakiwa kumwambia ni NISAMEHE MKE WANGU AU
NISAMEHE MUME WANGU. Kwa kutamka maneno hayo wala huwezi kupungukiwa na
chochote na badala yake utakuwa unaokoa penzi lako lisinyauke.
Kuwa mwepesi wa kuomba msamaha pale
unapokosea kwani mbali na kwamba inaonesha utu lakini pia inadhihirisha kuwa
huyo uliyenaye unampenda na huna dhamira ya kumkwaza.
Tuache ubabe wa kutojali
hisia za wenza wetu maana madhara yake ni makubwa ikiwemo penzi kufa.
Mbali na hayo, kuna hili neno ASANTE! Wakati
mwingine unaweza kukuta mume anafanya jambo zuri kwa ajili ya mke wake lakini
wala mke haoneshi kuthamini kwa kushukuru.
Anaona kwa kuwa aliyemfanyia ni mume
wake, ni wajibu wake hivyo haina haja ya kushukuru.
Kama wewe ni kati ya wanawake hao basi huijui
nguvu ya kushukuru. Kumbuka kwamba hata kama ni mumeo lakini akikununulia
zawadi, kusema asante inampa nguvu ya siku nyingine kukuletea.
Kumbuka wapo
ambao wako kwenye ndoa kama wewe lakini waume zao wala hawawafanyii wake zao
mambo hayo.
Hata mnapokuwa kwenye uwanja wa mahaba, nazungumzia faragha. Kama mume
amekupa raha uliyokuwa unaitaka, kusema ASANTE MUME WANGU kwa penzi nono,
kunanogesha penzi na kutamfanya kila wakati akufurahishe. Kwani ukitamka hivyo
unapungukiwa nini? Anza leo tabia ya kushukuru, hiyo itakuwa sehemu ya mbolea
ya kulistawisha penzi lako.
EmoticonEmoticon