Mtakubaliana nami kuwa suala la kuwa na wivu kwa mpenzi wako ni jambo
lisilokwepeka hasa kwa sababu kubwa ya kuaminika kwake kwamba kuwa na wivu ni
moja ya kigezo cha kuonesha ni jinsi gani unampenda mpenzio na kwamba hauko
tayari kwa namna yoyote ile kushea na mwingine, ndio maana wanawake wengi
hawataki kusikia suala la ukewenza kabisaa! Hata kama jambo hilo limepewa
baraka zote na dini au tamaduni zao.
Lakini kubwa katika wivu ni ile
kutokuwa tayari kuona tunasalitiwa na wapenzi na hasa kwa wale tunaowapenda
ukweli toka moyoni mwetu na zaidi ukute ndo tumeshawa-gharamikia kiasi cha
kutosha na kujitoa kwao kwa kila kitu!
Umeshawahi
kusikia kauli kama ‘Jamani mke (au mume) anauma! Au kauli kama mke wa mtu sumu”
na hugeuka sumu kweli pale unapobambwa na mali za wenyewe, kufanyiwa kitu mbaya
inakuwa sio jambo la ajabu sana.
Nikuambie tu kwamba, mapenzi ni full uchoyo,
ni full kujipendelea! Mpenzi wanaume kwa mfano, anaweza kufikiria kwamba ni
yeye tu ndiye anayestahili na anayeweza kumfanya mpenzi wake acheke na kufurahi.
Na kwamba
akitokea mwanaume mwingine akapata nafasi ya kumfurahisha mpenzi huyo hata
katika stori za kawaida tu, unaweza ukasikia akisema, ‘Hivi wewe mna nini na
huyo jamaa, mbona unamchekea chekea hivyo, au…!’
Hiyo ndiyo choyo ya penzi na
kikubwa kinachofanyika hapo ni ile tu kujaribu kulinda maslahi binafsi.
Pamoja na
ukweli kwamba tabia ya wivu inapozidi hugeuka kuwa kero, lakini kabla
hatujafika huko hebu tuangalie nafasi ya wivu katika mapenzi yetu.
Yaani swali
ni kwamba, je! Wivu katika mapenzi unaleta maana? Nionavyo mimi wivu ukitumika
vizuri unaleta maana na una nafasi muhimu sana katika mapenzi kwa sababu
zifuatazo:
1.Huonyesha kujali.
Sote
tunaamini pasipo na wivu hata chembe, hapana mapenzi ya kweli. Kumuonesha wivu
mpenzi wako ni kumjulisha ni kiasi gani unamjali na kumpenda na kwamba yeye ni
mtu maalum sana kwako.
2.Wivu unaonyesha kuthamini uhusiano.
Kwa mfano
unaweza kumsikia mtu akisema;
“Sio kama
sikuamini dear, bali wivu wangu kwako ni katika kuuthamini uhusiano wetu, mimi
na wewe ni umoja wenye thamani kubwa, tusiruhusu kuuchezea nje yetu! Huu ni
mfano wa ujumbe unaoonesha maana na nafasi ya wivu katika mahusiano ya
kimapenzi.
3.Wivu unaleta mazingira ya kujijengea heshima.
Kwa mfano mume
mwenye wivu na mkewe hujijengea heshima ya kwamba kweli anamjali na kumpenda
mkewe lakini pia anaweka mazingira ya kutosumbuliwa kwa mke wake huyo.
EmoticonEmoticon