Wayne Rooney Anaisubiri Nafasi Ya Kutangazwa Kocha Mpya Wa Derby County

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney anajiandaa kutangazwa kocha mpya wa Derby County muda mfupi ujao.
Mbali na kutangazwa kocha, Rooney (33) atakuwa mchezaji wa timu ya Ligi Daraja la Kwanza England.
Rooney anakwenda kujaza nafasi ya Frank Lampard alirejea England kuinoa Chelsea.
Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuachana na klabu yake ya DC United ya Ligi Kuu Marekani.
Rooney amebakiza miezi 13 kabla ya mkataba wake wa miaka mitatu DC United kumalizika.
Ingawa mkataba wake unamalizika mwakani, lakini wakala wake Paul Stretford, amemaliza mazungumza ya awali na vigogo wa Derby.


EmoticonEmoticon