Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu
pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo
mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo.
Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya
ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii.
Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi
fahamu faida 25 za kutembea kwa miguu.
1.Hukabili maradhi ya moyo kwa
kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
2.Huimarisha mifupa.
3.Huondoa au kupunguza hatari ya
kupata kiharusi.
4.Husaidia kupunguza uzito.
5.Huzuia saratani ya utumbo mpana.
6.Hukuwezesha kupata vitamini D
kutoka kwenye jua.
7.Hukusaidia kuboresha usawa wa
mwili wako (balance).
8.Hukabili maradhi ya kisukari.
Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta uwiano wa urefu na uzito – BMI; jambo
litakalokukinga na aina ya pili ya kisukari (Type 2 Diabets).
9.Hukabili shinikizo la damu.
10.Huondoa msongo wa mawazo.
11.Huongeza utayari.
12.Hukufanya ujifunze mambo
mbalimbali kwa kuona.
13.Hukuokolea gharama za nauli au
mafuta.
14.Hupunguza lehemu mbaya mwilini
(cholesterol)
15.Huimarisha misuli.
16.Husaidia mmeng’enyo wa chakula
kwenda vizuri.
17.Huwezesha kinga mwili
kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
18.Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
19.Hukujengea mahusiano ya kijamii.
Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
20.Huzuia kuzeeka. Utafiti
uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
21.Hukuweka katika hali nzuri
(mood).
22.Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka
mazoezi ni chanzo cha usingizi
mzuri.
23.Huboresha afya ya uzazi hasa kwa
wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya
uzazi.
24.Huzuia kuharibika kwa mimba.
Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo
zoezi rahisi na jepesi kwake ni kutembea.
25.Huboresha mwonekano wa mwili.
Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya mwili wako uonekane katika umbo zuri.
Hivyo kutembea kama aina mojawapo ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.
USHAURI.
Inashauriwa kuhakikisha unatembea kwa miguu angalau dakika 30 kila siku.
Kwa njia hii utapata manufaa mengi yaliyotajwa hapo juu.
EmoticonEmoticon