Adele Awasilisha Maombi Ya Talaka

Mwimbaji wa muziki Adele amewasilisha kesi ya talaka dhidi ya mme wake Simon Konecki, kwa mujibu wa nyaraka za kesi zilizowasilishwa katika mahakama nchini Marekani
Mwakilishi wao amesema kuwa wawili hao " wako tayari kushirikiana kwa pamoja kumkuza mtoto wao mpendwa wa kiume ".
Adele alijifungua mtoto wa kiume , Angelo, mnamo mwaka 2012. Aliolewa na Konecki - ambaye ni mwekezaji katika sekta ya benki ambaye aligeuka na kuwa mkuu wa shirika la misaada mwaka 2016 baada ya miaka mitano ya uchumba.

Taarifa kuhusu maombi yake ya talaka iliongeza kuwa wawili hao ambao walitangaza kuachana mwezi Aprili waliomba kesi yao iwe ya siri na kwamba hawatatoa maelezo yoyote. Karatasi za talaka ziliwasilishwa katika mahakama mjini Los Angeles.

Ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa Adeleanarekodi muziki mpya , na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 31- alipigwa picha akielekea katika studio kurekodi muziki katika studio mjini New York City mwezi Machi


EmoticonEmoticon