Akon Ataja Tabia Ya Eminem Katikati Ya Mahojiano (VIDEO)

Mwanamuziki Akon alikaa kwenye meza ya mahojiano nakituo cha redio cha Hot 97 nakuzungumzia mambo mengi ikiwemo uzoefu wake wakufanya kazi na rapa Eminem.

Katika mazungumzo yake Akon alisema hajawahi kukutana na msanii mwenye nidhamu ya kazi kama Eminem kwani aliufanya muziki wake kuwa maana halisi ya biashara kwa kuzingatia muda pindi anapohitajika studio kitu ambacho ni tofauti na wasanii wengine.

Akon na Eminem wamewahi kufanya pamoja ngoma ya "Smack That" iliyotoka mwaka 2006 ambayo ilikuwa inapatikana kwenye albam ya Akon ya Konvicted.


TAZAMA MAHOJIANO HAPA


EmoticonEmoticon