Alichokiandika CR7 Baada Ya Kukosa Kwenye Tuzo Za Fifa

Cristiano Ronaldo
Jumatatu usiku wa September 23, kulikuwa na usiku wa tuzo ambapo kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa soka ulimwenguni waliweza kushuhudia baadhi ya watu wakifanikiwa kuondoka na tuzo huku macho na masikio ya walio wengi yalikuwa yakiangazia kwa nafasi ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA 2019 kipengele ambacho kinawakutanisha mahasimu wawili na wanasoka bora na vipenzi wa mashabiki Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ukiachia mbali Virgil van Dijk akiwemo kwenye kipengele hicho.

Katika usiku huo maalum ambao ulihudhuriwa na wanasoka mbalimbali ulishuhudiwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA 2019 na kumpiku beki wa Liverpool, Virgil van Dijk pamoja na hasimu wake Ronaldo.

Ronaldo aliposti picha usiku huo kupitia akaunti yake ya Instagram inayomuonesha akiwa nyumbani kwake akijisomea kitabu huku akiandika ”Uvumilivu na kutokukata tamaa ni sifa mbili ambazo zinazomtofautisha mtu ‘professional na amateur’.”
CR7 Instagram Post
Messi ulikuwa usiku wa fura mno kwa upande wake baada ya kutwaa tujzo hiyo hasa kutona na kazi kubwa aliyofanya msimu uliyopita wa 2018/19 akifunga jumla ya mabao 54 kwenye michezo 58 aliyocheza na kutoa pasi za mwisho 20 zilizochangia kupatikana kwa magoli.
Hata hivyo Ronaldo mwenye miaka 34, amefunga jumla ya magoli 31 katika michezo 47 aliyocheza msimu uliyomalizika wa mwaka 2018/19.


EmoticonEmoticon