Beef La Mane Na Mo Salah Limefikia Hapa

Mane akitulizwa na Kocha
Sadio Mane amesema amemaliza tofauti zake na Mohamed Salah baada ya kutokea mzozo baina yake katika mechi dhidi ya Burnley.

Mshambuliaji huyo wa Senegal, alisema alikutana uso kwa uso na Salah na wamekubaliana kumaliza tofauti zao.

Mane aling’aka mbele ya Kocha Jurgen Klopp alipotolewa katika mchezo huo baada ya Salah kumtaka kurekebisha kasoro akiwa ndani  ya eneo la hatari.

Mane hakufurahishwa na maelekezo ya nahodha huyo wa Misri na mara moja alimshambulia kwa maneno makali.
Kinara huyo wa mabao, alivua jezi na kuitupa chini alipokuwa katika benchi.

“Nini kuhusu Salah? Yamepita hayo,” alisema Mane baada ya kumalizika mchezo wa Ligi Kuu England walioshinda mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United.

Maelewano Mazuri yaliyopo kati ya Mane & Salah

Mchezaji huyo alisema kutofautiana kauli uwanjani ni jambo la kawaida na mara nyingi linatokea,” alisema Mane.

Nyota huyo alisema wamerejesha urafiki wao kama zamani na mkakati uliopo mbele yao ni kuipa mafanikio Liverpool.

Liverpool itasafiri kwenda Italia kuivaa Napoli katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa UIaya Jumanne kabla ya kuivaa Chelsea, Jumapili.


EmoticonEmoticon