Cristiano Ronaldo Akiri Mipango Ya Kufunga Ndoa Na Mrembo Huyu

Cristiano Na Georgina Rodriguez

Cristiano Ronaldo ameamua kufunguka bayana kuhusu mpango wa kufunga ndoa na mrembo Georgina Rodriguez.

Fowadi huyo wa Juventus mwenye umri wa miaka 34, amekuwa kwenye uhusiano na mrembo Georgina mwenye miaka 25 tangu mwaka 2016.

CR7 Na Familia Yake
Uhusiano huo umeleta matunda ya binti mmoja, lakini kinachomfurahisha Ronaldo ni kuhusu Georgina alivyokuwa na moyo wa kuwalea watoto wengine watatu wa Ronaldo bila ya kinyongo chochote.

Ronaldo alisema mpango wake ni kumwoa mrembo huyo licha ya kwamba hakutaka kusema ni lini jambo hilo litafanyika.

Akizungumza kwenye mahojiano aliyofanyiwa na Piers Morgan, ambayo yalirushwa hewani Jumanne iliyopita, Ronaldo alisema: "Sote tutafunga ndoa siku moja, kwa hakika.
Hiyo ni ndoto ya mama yangu pia. Hivyo, siku moja nitaoa, kwanini isiwe?"
Wakiwa matembezi na familia
Mrembo, Georgina, aliyezaliwa na mama Mhispaniola na baba Muargentina alikutana na Ronaldo wakati huo alipokuwa akiichezea Real Madrid.

Na sasa anaishi na mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or huko Turin, Italia na watoto wao Cristiano Jr (8), pacha Eva na Mateo (2) na binti wao Alana Martina (1).
Wakiwa matembezi na familia
Mrembo Georgina alisema alipendana na Ronaldo baada ya kuonana naye siku ya kwanza tu huko kwenye duka la Gucci.


EmoticonEmoticon