Cristiano Ronaldo Alitaka Familia Yake Isifahamu Kesi Ya Madai Ya Ubakaji

CR7 Na Mchumba wake Georgina
Nyota wa soka Cristinao Ronaldo amesimulia jinsi tuhuma za ubakaji zilimweka katika hali ya utata na aibu.

Ronaldo amesema kuwa alihisi fedheha kubwa sana.Juhudi zilikuwa nyingi za kuificha familia yake dhidi ya madai haya.

Ronaldo alishtumiwa kumbaka mwanadada Kathryn katika hoteli moja eno la Las Vegas Juni 2009.

Nyota huyu alipata afueni baada ya waendesha mashataka kusema kuwa madai hayo hayakuwa na msingi wowote wa kisheria kulingana na mchezaji huyu wa soka.
Cristiano na Familia yake
Kashfa ya kumhusisha katika swala la ubakaji ilimzonga sana kimawazo na hakutaka familia hususan watoto wake wafahamu kisa hiki.

“Watu wanaichezea sana hadhi yako.’ Alisema Ronaldo
“Mpaka nakumbuka siku moja nimetulia sebuleni na mpenzi wangu tukitazama habari za runinga na zikaja zile taarifa.” Aliendelea kusimulia

“Ghafla nikawasikia watoto wangu wakiteremka kuja sebuleni nikabadilisha channel, nilibadilisha kwa sababu sikutaka Ronaldo Jnr atazame babake akihusishwa na kesi mbaya.”


EmoticonEmoticon