DMX Asaini Dili Hili Jipya

Dmx
Taarifa mpya zinasema kwamba rapper huyo mkongwe amesaini dili jipya na Label ya Def Jam Records.

Pia mtayarishaji na rapper Swizz Beatz amethibitisha hilo kwenye mahojiano yake na The Breakfast Club wiki hii, alisema "Huu utakuwa mwaka mzuri kwa DMX kama Mungu akipenda, Ninataka hilo litokee ili aweze kurejea kule alipotakiwa kuwepo."


View this post on Instagram

A post shared by DMX (@dmx) on

Chini ya Def Jam Records, DMX alifanikiwa kuachia album kali kwa muda wote. Kwa miezi tofauti mwaka 1998 X' aliachia album mbili "It’s Dark and Hell Is Hot" na "Flesh of My Flesh, Blood of My Blood." ambazo zote zilikamata namba 1 kwenye Billboard 200.


EmoticonEmoticon