Facebook Inatambua Mtu Aliyetoka Kufanya Mapenzi

Taarifa binafsi na siri zikiwa pamoja na wakati ambao watu wanafanya mapenzi zinaonyeshwa katika mtandao wa Facebook, utafiti uliofanywa 'Privacy International' umeeleza.
Utafiti huo umeonyesha namna ambavyo programu iliweza kuona taarifa zote ambazo ziliandikwa katika mitandao.Hii ikijumlisha taarifa kama ya siku ambazo mtu alitumia dawa za mpango wa uzazi, siku zake za hedhi na dalili alizokuwa anazipata.
vitu ambavyo Facebook inaviona - "Lengo : Kupata ujauzito"

Tangu utafiti huo ufanyike, programu moja imesema kuwa imebadili sera zake za siri.

Programu ya mzunguko wa hedhi inahifadhi taarifa ambazo ni binafsi sana kwa mtu kama vile hali ya afya yake, ngono, hisia zake, chakula anachokula na pedi anazotumia.
Na pogramu hiyo huwa inamuelekeza siku za miezi ambazo anatarajia kupata hedhi yake.

Kushirikisha Facebook kwa kutumia programu kunaweza kufanya wapate fedha kutokana na matangazo ambayo yanawekwa.

Programu ya Maya inawahamasisha watumiaji wa programu yao kuingiza taarifa za jinsi wanavyojisikia na kuweka kwenye Facebook

BBC imejaribu kuwasiliana na kampuni hizo na hakuna aliyetoa jibu lolote.
Utafiti huo unaamini kuwa hilo suala linaleta hofu kwa watumiaji wa programu hizo kwa kuwa umeshindwa kutunza siri za taarifa zao.
Na wa husika wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwaaminisha watumiaji jambo ambalo si la kweli.
Facebook imetangaza kuanzisha programu yake na kuachana na biashara za kushirikiana na wengine katika mtandao huo.

SOURCE:BBCSWAHILI


EmoticonEmoticon