Hii Ndyo Kampuni Iliyomfanya Pogba Kutoondoka Man U

Kampuni ya Vifaa vya Michezo ya Adidas ndio iliyoingilia kati na kuzuia uhamisho wa staa wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba kutoka Manchester United kwenda Real Madrid katika dirisha kubwa lililopita.

Adidas ina mkataba na Manchester United pamoja na kiungo huyo na ilifanya kikao cha amani baina yao baada ya staa huyo kutangaza kuondoka klabuni hapo wakati akiwa katika ziara yake ya kibiashara kule Japan.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa alisema alihitaji kupata changamoto nyingine nje ya Manchesta United.

Pogba ameanza mechi zote nne za Manchester United msimu huu na amepika mabao mawili lakini bado anatazamiwa kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huku Madrid pia ikiwa imepania kumtwaa staa huyo.

Inadaiwa Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ndiye aliyekuwa chachu ya Mfaransa mwenzake huyo kutaka kutua Santiago Bernabeu.


EmoticonEmoticon