Jose Mourinho Aongelea Hali Ya Manchester United Kuporomoka

Jose Mourinho
Jose Mourinho amekiri kuwa alistahili kufukuzwa ukocha katika kikosi cha Manchester United, lakini akasisitiza kuwa hafurahii kuwaona wakiendelea kuteseka chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.

United walichapwa 2-0 na West Ham juzi Jumapili, matokeo yaliyowafanya waporomoke hadi nafasi ya nane kwenye msimamo.


Klabu hiyo ilikuwa nafasi ya sita wakati Mourinho alipotimuliwa katikati ya msimu uliopita baada ya mashabiki kuchukizwa na soka lake la kujilinda sana.


“Mimi siyo mtu sahihi kujibu hilo,” alisema Mourinho alipoulizwa matatizo ya Manchester United ni yapi. “Wako mbali sana. Ni ngumu mimi kujibu.


Nilikuwa pale kwa misimu miwili ambako niliona vitu vingi chanya na mwelekeo ulikuwepo, baadaye msimu wa tatu haukuwa mzuri sana.


“Nilifukuzwa. Pengine nilistahili kufukuzwa kwa sababu nilikuwa nawajibika kama kocha, lakini ukweli mchungu ni kwamba wamekuwa hovyo kuliko wakati ule.


Na kwangu mimi, hicho ni kitu kibaya. Pengine watu wanadhani nafurahia hali hii lakini sifurahii kabisa.” Mourinho amesema anaamini Manchester United itapata shida hata kuingia kwenye top 6.


EmoticonEmoticon