Kiwango Cha Mapato Ya Manchester United, Kimepanda Au Kimeshuka?

Man U Team
Mapato ya Manchester United yameongezeka kwa rekodi mpya ya kiwango cha £627m kwa mwaka kufikia Julai.
Hii ni licha ya klabu hiyo kukabiliwa na msimu mgumu wa 2018-19 liochangia kuondoka kwa meneja Jose Mourinho na timu hiyo kumaliza msimu ikiwa katika nafasi ya sita.
Mapato yanayotokana na matangazo ya biashara yaliimarika kwa 18%, kutokana na mkataba mpya wa Uefa ya ligi ya mabingwa, huku mauzo ya kibiashara yakisalia kama yalivyokuwa.
Lakini timu hiyo inatarajia mapato na faida kushuka katika msimu wa 2019-20 baada ya kushindwa kufuzu katika ligi ya mabingwa msimu huu.
Klabu hiyo kwa sasa ni ya nane katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kuanza msimu kwa mchezo wa kiwango cha chini.
Inaiwacha nyuma ya Liverpool kwa pointi 10 na pointi tano nyuma ya mahasimu wa mjini na mabingwa watetezi Manchester City.
Kuna hatari kwa klabu hiyo kuishia nyuma ya wapinzani wake wa miaka mingi Ulaya kuipata haki ya kutambulika kuwa Klabu tajiri duniani.
Wiki iliyopita mabingwa wa Uhispania Barcelona walitangaza wanatarajia kupitisha kiwango cha mapato ya thamani ya £883m kwa mara ya kwanza msimu huu


EmoticonEmoticon