Klopp, Van Dijk Wawekewa Tageti Huko Hispania

Jurgen Klopp na Virgil van Dijk
Jurgen Klopp na beki wake Virgil van Dijk wote wamewekwa mtu kati na klabu za Hispania, Barcelona na Real Madrid wakitaka huduma zao na huenda hilo likafanyika kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwakani.

Jambo hilo linawaweka kwenye presha kubwa Liverpool, ambao bila ya shaka watakuwa kwenye presha kubwa kama watawapoteza watu wao hao wawili muhimu kabisa.

Klopp na Van Dijk wamekuwa watu muhimu kwenye mafanikio ya Liverpool kwa miaka ya karibuni, lakini vigogo hao wa Hispania wanataka kujiimarisha zaidi na kuamini huduma za wakali hao zitakuwa na faida kubwa kwenye vikosi vyao.


EmoticonEmoticon