Kocha Aeleza Hali Ya Messi Baada Ya Kuumia Uwanjani

Messi akiuguzwa Majeraha na Doctor
Lionel Messi ameumia tena katika mchezo  wake wa kwanza akitokea katika majeruhi.

Nahodha huyo wa Barcelona, aliumia mguu katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Villarreal kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Nyota huyo amepata majeraha muda mfupi baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia aliyopata katika hafla ya mjini Milan, Italia.
Lionel Messi
Messi aliyecheza mechi yake ya 400 juzi usiku, alishuhudia timu yake ikipata ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Antoine Griezmann na Arthur.

Bao la Villarreal lilifungwa na nyota wa zamani wa Arsena, Santi Cazorla.

Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde alisema nahodha huyo wa Argentina hakupata maumivu makubwa.
Kocha Wa Barcelona Ernesto Valverde
“Amepata maumivu kidogo, unajua tukio lolote linalompata Messi kila mmoja anashituka, tutaangalia afya yake,”alisema kocha.


EmoticonEmoticon