Kocha Wa Man U Afunguka Haya Juu Ya Timu Yake Baada Ya Kusemwa Sana

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba kikosi chake chenye wachezaji wa umri mdogo kinaimarika kila uchao ikilinganishwa na vile walivyoanza msimu.
United imeshinda mara moja katika mechi zake tano za ligi ya Uingereza na ilihitaji penalti kuishinda klabu ya daraja la kwanza ya Rochdale katika michuano ya Carabao siku ya Jumatano.
''Sijasema kwamba itakuwa rahisi msimu huu'' , alisema mkufunzi huyo wa Man United.
''Kutakuwa na changamoto. Tunaposhindwa mechi lazima tujiamini na kile tunachofanya''.
Kikosi hicho cha Solkjaer ambacho kilishindwa 2-0 na West Ham wikendi iliopita , kitachuana na Arsenal katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumatatu usiku.
''Utamaduni upo, hatuna tatizo na jinsi wachezaji wanachukulia kila mechi, na viwango'' , aliongezea.
''Unaweza kuona dhidi ya Astana na Rochdale, wanataka kucheza vizuri na mara nyengine wanaharakisha mashambulizi yao''.
''Mechi yoyote katika ligi ya Premia inaweza tukashinda na pia tunaweza kupoteza'', alisema Solskjaer.
Mara nyengine unasimama uwanjani ukiwa na furaha kwa kushinda mechi , mara nyengine umekasirika kwa kuwa umepoteza. Lazima tuonyesha picha nzuri''.
''Unaweza kuona jinsi tulivyoimarika katika safu ya ulinzi hapo ndipo tunapowekeza huku Aaron Bissaka na Harry Maguire wakiweka ulinzi wa kutosha. Hatufungwi magoli mengi''.
''Tukisonga mbele, hiyo ndio safu iliokumbwa na majeraha chungu nzima. Paul Pogba, Anthony Martial, Marcus Rashford - tumekuwa na bahati mbaya. Haisaidii unapopoteza wachezaji - vijana hawa wanahitaji kupata mfumo wa kucheza''.
Solskjaer aliwashukuru mashabiki, ambao kikosi chao kilimaliza katika nafasi tatu za kwanza katika ligi ya Premia mara moja katika kipindi cha misimu sita iliopita na kutoa wito kwa mashabiki kuendelea kuisaidia timu hiyo


EmoticonEmoticon