Kocha Zidane Apunguza Machungu

Mshambuliaji nguli, Karim Benzema amempa raha Zinedine Zidane baada ya kufunga bao pekee la Real Madrid ikishinda 1-0 dhidi ya Sevilla.

Nyota huyo wa Ufaransa, alifunga bao hilo kwa kichwa katika mazingira magumu akiwa ndani ya eneo la hatari la wapinzani wao.

Ushindi huo umepoza machungu ya Zidane ambaye alipoteza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya timu yake kulala mabao 3-0 dhidi ya Paris Saint Germain (PSG).

Idadi kubwa ya mashabiki walichukizwa na matokeo hayo, lakini Zidane aliahidi kulipa kisasi dhidi ya Sevilla.

Pia matokeo hayo yaliibua tetesi ya kocha huyo kutupiwa virago huku nafasi yake ikitajwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo Xabi Alonso.

Sevilla inanolewa na kocha wa zamani wa Real Madrid, Julen Lopetegui, aliyefukuzwa baada ya kuinoa kwa miezi minne na nusu tu baada ya kupata matokeo mabaya.


EmoticonEmoticon