Kufanya Mapenzi Kila Siku, Wataalamu Wanaushauri Gani?


Kuna watu ambao hawawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.

Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida Nyingi, lakini linapo kuja swala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.

Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kilia siku ‘anahondomola’ kwa sababu tu hakuna wakumkataza na kwamba anahaki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.

Imeelezwa kuwa watu wengi kati ya watu wanao lalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.

Si kila unapokutana na mwenza wako basi mshiriki tendo la ndoa kwani kwani kufanya hivyo ni sawa na kujikomoa mwenywe. Miongoni mwa madhara ni pamoja na;-

Kupoteza hamu ya tendo

Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kufanya mapenzi kwa wenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinaweza kujitokeza wakati wa kufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

Sababu hizo ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi chakukosa msisimko hata Anapo muona akiwa mtupu.

Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza. Kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi napengine kitanda kimoja au chumba kile kile ,jambo ambalo linaweza kumfanya muhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo hupoteza hamu naye na kihisi kama hawezi kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

Kuujaza mwili tamaa kubwa
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo humfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya nae mapenzi na kwa wakati gani.

Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndio wale ambao kila wanae mtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake au afya yake.

Unakuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wakuizuia tamaa yako mwenza wako akiondoka siku mbili utatamani uwe na yeyote aliye karibu yako ili akukate kiu ya penzi.

Kupoteza raha kamili ya tendo
Raha ya tendo hutegemea na hisia iliyo kuzwa kutokana na mapenzi sahihi au kuwa na kiu ya kufanya mapenzi,hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.

Kama ni mapenzi utakua unafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo.

Kupoteza nguvu za mwili


Madhara mengine yanayo weza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.

Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi,hivyo huufanya mwili uchoke.

Aidha lishe inapo kuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.

Sambamba na hivyo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wafanyao mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

Kupata magonjwa

Wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa holela ambayo huweza kuwa sabababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi,lakini ufanyaji wa mapenzi usiyo kuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wana wake huwa fanya waishiwe misisimko na huzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unao weza kuwakinga na michubuko wakati wakujamiiana na hivyo huwa sababishia michubuko itayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa na ukimwi ukiwemo.


EmoticonEmoticon