Kuondoa Tatizo La Harufu Mbaya Ukeni

Harufu mbaya ukeni, inaweza kuwa kama shombo la samaki alieharibika Ute wa kijivu, mweupe au njano, Muwasho ukeni, Maumivu wakati wa kukojoa n.k

Namna Ya Kuondoa Tatizo hili

1.Epuka kusafisha uke hadi ndani
Sawa utaona inaondoa uchafu,ila haikusaidii bali inaondoa Zaidi hali ya Asidi ya uke na kupelekea kuongeza tatizo la harufu mbaya ukeni

2.Pata matibabu ya Bacteria vaginosis

3.Kunywa mtindi.
Mtindi una bakteria wazuri wanaosaidia kuweka uke katika hali yake wanajulikana kitaalamu kama PROBIOTICS.Unapokunywa mtindi inasaidia kuweka hali ya uke katika usawa na kukukinga na magonjwa kama fangasi za ukeni na vaginosis

4.VAA NGUO ZA NDANI ZENYE ASILI YA PAMBA(COTTON)
Pamba(cotton) ina uwezo wa kupitisha hewa hata kama ni kidogo sana. Na sehemu za siri za Mwanamke zinahitaji flow ya hewa inayopita,nyingine iwe inaingia na nyingine iwe inatoka.Hii flow ya hewa hata kama ni ndogo itasaidia kufanya sehemu zako za siri kuwa fresh muda wote na utapunguza uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.
Na pia punguza kuvaa nguo za kubana sana muda wote,nguo za kubana zinasababisha majasho sehemu za siri na ukizingatia hamna flow ya hewa kwenye sehemu zako za siri basi lazima hayo majasho yataanza kutoa harufu mbaya.

5.USIVAE NGUO YA NDANI MOJA SIKU NZIMA

Kwa jinsi maumbile ya Mwanamke yalivyo,unatakiwa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku.
May b ulivaa nguo ya ndani asubuhi,ikifika mchana,ingia ladies room(bafuni/chooni),Vua Nguo yako ya Ndani,kisha unaweza ukaoga mwili mzima(which is better) au ukasafisha sehemu zako za siri.Nguo ya ndani uliyovua unaweza ukaifua(which is better) au ukaikunjakunja na kuiweka ndani ya kipande cha khanga au kitenge ndio uweke kwenye handbag yako ili kama ikitokea ukaopen handbag yako in public,watu wataona khanga au kitenge,hawatojua ndani umeweka nini.

6.PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI AU YEAST KWA WINGI

Unaweza ukapunguza uwezekano wa kupata Yeast Infection au Bacteral Vaginosis kwa kuacha au kupunguza kula vyakula vyote vyenye sukari au yeast kwa wingi.

Vyakula hivyo ni kama vile vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe/bia n.k
Ukizidisha Vyakula au vinywaji hivi,ina maana utakuwa unazidisha yeast mwilini,na wakizidi kwenye uke utapata yeast Infection,mwisho wake uke wako utaanza kutoa harufu mbaya.

7.BADILI PADS ZAKO MARA KWA MARA UNAPOKUWA KWENYE SIKU ZAKO

Ili kuzuia uke wako usitoe harufu mbaya kipindi ambacho upo kwenye siku zako,inashauriwa kubadili ur pad mara kwa mara(may b after each 4 or 6 or 8 hours,it will depend how many pads can u afford per day).

Kubadili pads mara kwa mara kunasaidia ujisikie upo comfortable,inazuia bacteria kujikusanya,inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata infection na mwisho inaondoa uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.

MATIBABU YA NYUMBANI.
Endapo unasumbuliwa mara kwa mara na Tatizo la harufu ukeni, au unapata matatizo kama fangas za ukeni mara kwa mara na UTI zingatia hapa.

Bila shaka umesikia mengi mfano,
Kuweka limao ukeni
Kuweka kitunguu saumu
Kuweka Bicarbonate nk.

Ila ukweli ni kwamba Unachohitaji ni kuweka PH ya uke wako kati ya 3.8 hadi 4.5 ndo itakua suruhisho la tatizo lako. Kama tayari umeshapata Fangas za ukeni au Bakteria vaginosis inapaswa Upatiwe matibabu kwanza ndo ubalance PH ya uke ili kuzuia tatizo lisitokee tena.

KUHUSU LIMAO
Wengi hudai Kwamba limao au kuweka juisi ya limao ukeni inatibu fangasi za ukeni na inatibu Fangasi na UTI.

Limao haitibu fangasi wala bakteria. Limao ndani yake ina Asidi ya PH ya 4.2, Tafiti zinaonesha unapoweka juisi hii kwenye uke inaongeza PH kwa kiwango cha 0.2 zaidi. 

Ila Limao ina vitu vingine ndani yake.Inapomeng’enywa viambata vyake vinapovunjwa vunjwa vinatengeneza end products ambazo zina PH ya 8.9 yaani Hali ya nyongo (basic) hivyo kupandisha tena PH ya uke. 

Pia unapokunywa juice yake inapofikia kutolewa kwenye mkojo  huwa si aside tena inaongeza PH ya mkojo. 

Kwa hiyo juice ya limao unapoiweka ukeni Katika dakika za mwanzo inaopunguza PH ya uke kwa 0.2 yaani kama iliku 7.2 itakua 7 na kuendelea ila baada ya muda bakteria wa ukeni wanapoanza kuivunja vunja inaongeza PH hadi 7.5 hadi 8.5. Kwa hiyo haisaidii.

KUHUSU BICARBONATE NA KITUNGUU SAUMU
Kwa kuanza na kitunguu saumu ndani yake kina Allicin hiyo inayokipa harufu yake.Allicini ni nyongo (base) ina PH ya 7.9, hivyo inapotumika haisaidii bali I naongeza tu PH ya uke kuwa Basic.

Bicarbonate yenyewe hii pia ni nyongo,ukiweka unaongeza PH ya uke na kuongeza hali ya nyongo (basic) ya uke hivyo kuzidisha tatizo.


EmoticonEmoticon