Maneno Ya Messi, Neymar Kurudi Barcelona

Lionel Messi anasema "angependa" Neymar kurudi Barcelona kwani kuwasili kwake kungekuwa "kumeongeza nafasi ya kufikia malengo yetu."
Neymar, 27, alijiunga na Paris St-Germain kutoka Barcelona mnamo 2017 kwa ada ya rekodi ya dunia ya euro 222m (£ 200m).
"Alitamani sana kurudi," Messi aliliambia gazeti la Spoti la Uhispania. "Sijui kama kilabu kilijaribu kweli au la."
Neymar alifunga mabao 105 katika michezo 186 kwa kilabu cha Catalan kati ya 2013-2017, na ana magoli 51 katika michezo 58 aliyoichezea PSG.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Brazil alihusishwa mara kwa mara na taarifa za kurudi Barcelona wakati wa dirisha la usajili, ingawa imedaiwa kwamba hakuna kilabu chochote ambacho kilishawishika.
"Ningependa Neymar arudi," alisema nahodha wa Barcelona Messi, 32. "Ninaelewa watu hao ambao wanapingana na kurudi kwake na inaeleweka kwa kile kilichotokea kwa 'Ney' na namna ambavyo aliondoka.
"Lakini nikifikiria juu ya kiwango cha mchezo wake, mimi binafsi nadhani Neymar ni mmoja wa wachezaji bora ulimwenguni na kuwa naye kwenye kikosi chetu kutaongeza nafasi zetu za kufikia malengo yetu."
Messi alikataa madai kuwa wachezaji wa Barcelona waliiomba klabu hiyo kumsajili Neymar, na kuongeza: "Tulitoa maoni yetu kuwa itakuwa nzuri ikiwa atakuja lakini hatukuwahi kusema watalazimika kumsajili."
Licha ya kukosa kucheza kando na Mbrazili huyo tena, Messi alisema "hajasikitishwa", na kuongeza Barcelona kuwa na "kikosi bora na kinaweza kufanikiwa bila yeye."
Mshambuliaji huyo wa Argentina alijiunga na Barcelona mnamo 2001 na mkataba wake wa sasa unaisha mnamo Juni 2021.
"Wazo langu ni kukaa hapa kwa muda mrefu kama nina uwezo wa kucheza kwa kiwango kinachohitajika na mwili wangu unaruhusu," akaongeza.
"Hapa ni nyumbani kwangu. Sina mpango wa kuhamia mahali pengine tuendelee kushindana na kushinda."


EmoticonEmoticon