Maneno Ya Ramos Baada Ya Mpambano

Sergio Ramos
Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos amesema haikuwa kazi rahisi kuondoka na pointi moja katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Atletico Madrid kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano.

Real na Atletico Madrid zilishindwa kufungana kwenye mchezo huo wa mahasimu wa kwanza kuchezwa msimu huu wa 2019/20 baina yao.

“Ulikuwa mchezo mgumu sana uliohusisha matumizi ya nguvu kupita kiasi.  Uwanja ule ni kati ya viwanja vigumu karibu msimu mzima. Bao lingefunya kupata alama tatu, ilishindikana lakini jambo jema ni kutofungwa.

“Tulipata nafasi kupitia kwa Karim, lakini  Oblak aliokoa. Tulikuwa kwenye nafasi ya kushinda zaidi kuliko Atletico, tunatakiwa kuendelea kuonyesha kiwango kama hiki,” alisema


EmoticonEmoticon