Mashabiki Wataka Kocha Zidane Atimuliwe

Kocha Zidane
Magoli mawili ya Angel di Maria na moja la Thomas Manuer yalitosha kuipa PSG ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Real Madrid.
Huu ni mwendelzo wa matokeo mabaya kwa Madrid, na punde tu baada ya mchezo, mashabiki wenye hasira wenye klabu hiyo wakaanza kupiga mayowe wakitaka kocha wao Zinedine Zidane atimuliwe klabuni.
Kitu kibaya zaidi ni kuwa, licha ya PSG kupata ushindi huo mzuri, walikuwa hawana washambuliaji wao vinara wote watatu uwanjani; Neymar, Cavani na Mbappe.
Katika hesabu za nje ya uwanja, PSG ilikuwa dhaifu, lakini bado waliweza kuichakaza safu ya ulinzi ya Madrid.
Di Maria
Mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya kihistoria ni ulingo wa kujidai wa Madrid, wakiongoza rekodi ya kunyakua kombe hilo mara 13, lakini kiwango walichoonesha jana usiku kinawafanya wachambuzi kujiuliza iwapo watavuka hata hatua ya makundi.
Madrid katika mchezo huo wameshindwa kupiga walau hata shuti moja lililolenga lango, na hiyo inatokea kwa mara ya kwanza toka kampuni ya Opta ilipoanza kukusanya takwimu za mechi 2003-04.
Hiki ni kipigo kikubwa zaidi kwa Madrid katika mechi ya kwanza ya Klabu Bingwa (japo pia wameshapokea kipigo kama hicho mwaka 2004 na 2005 dhidi ya Bayer Leverkusen na Lyon mtawalia.
Kwa ujumla, PSG walimiliki mpira kwa asilimia 53 didi ya 47 za Real Madrid.


EmoticonEmoticon