Leo nipo upande wa kuwapa wanaume elimu ya maswali 10 ambayo wanatakiwa wajiulize ili kupima penzi lao kwa mtu aliyempenda, nikimaanisha mwanamke.
1.Anajitoa kwa ajili yako?
Mwanamke anayekupenda atakuwa tayari
kujitoa muhanga kwa ajili yako. Mwanamke anayekupenda atakua tayari kufanya
chochote kile kwa ajili yako kitu ambacho hawezi kufanya kwa ajili ya mtu
mwingine yoyote.
2.Atakupa kipaumbele?
Mwanamke anayekupenda atakupa kipaumbele katika vitu na mambo yake
yote. Mbele ya Marafiki zake wewe utakuwa ni bora zaidi.
3.Anakuchukulia
tofauti na wanaume wengine?
Mwanamke anayekupenda atakufanyia mambo ambayo hawezi kuwafanyia
wanaume wengine.
4.Anakupa nafasi
na muda wake?
Mwanamke anayekupenda anakupa nafasi na muda wake. Anauwezo wa
kuacha mabo mengine ili aweze kuwa na wewe.
5.Anakuhangaikia?
Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, Kawaida mwanamke
anayekupenda atahangaika juu ya usalama wako, raha yako, heshima yako na
maendeleo yako. Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke uliyemlenga
anakupenda kweli.
6.Ana wivu juu
yako?
Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa. Anaogopa usije
ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa. Wivu ni ishara kuwa
anakupenda wewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza, anaogopa
usije ukatoka katika maisha yake.
7.Anakushirikisha furaha yake?
Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu
wengine atacheka nao lakini atakugeuzia wewe macho namaanisha uso wake haraka
sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia wewe kuwa utaweza kumletea
furaha katika maisha yake, zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona
kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.
8.Anakuangalia
sana?
Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu
kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine, atakuangalia na kutabasamu vizuri.
Hii ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa anakuhitaji katika maisha
yake.
9.Anavaa vizuri mkutanapo?
Mwanamke anayekupenda atajitahidi apendekeze kwa kuvaa vizuri pale
anapojua kuwa atakutana na wewe, atajali sana juu ya nywele zake, nguo zake na
hata anavyonukia. Hii ni ili kukuvutia wewe na kuonyesha uwepo wake kwako.
10.Anapenda kuwa
karibu na wewe?
Mwanamke anayekupenda ataonyesha dalili za kupenda kuwa karibu
yako katika mazungumzo au maeneo mengine, atapenda mara nyingi kuwepo katika
maeneo unayopendelea na pia sauti yake itabadilika kuashiria hali ya kukupenda
na kutaka kukuvuta kwa sauti yake.
EmoticonEmoticon